Tuesday, 2 August 2016

Joh Makini amefunguka kuhusu kauli ya Chid Benz,kuwa yeye ametengezwa na media,fahamu zaidi..


Wiki kadhaa zimepita tangu msanii wa hip hop ,Chid Benz kusema kwamba hakuna msanii wa Hip Hop aliyefikia mafanikio yake na kudai kwamba wasanii kama Joh Makini na Nay wa Mitego wametengenezwa tu ili waje washike usukani lakini hawana nguvu.

Kwa upande wake Joh Makini alipoulizwa kuhusiana na kauli hiyo ya Chid kwenye kipindi cha funiko base cha radio 5 hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli hiyo na kuishia kusema kwamba anawahurumia sana watu kama hao wanaotumia muda wao kufanya mambo yasiyo ya msingi badala ya kufanya kazi.
kusema kweli mimi hainiumizi kabisa,kwa sababu kuna vitu siviruhusu kabisa na kila mtu ana jinsi anavyoishi na Mungu wake,sana sana mimi nawahurumia watu wanaowekeza kwenye hivyo vitu,kwa sababu naona jinsi gani wana struggle kwenye kupoteza muda kuliko kufanya kazi” alifunguka Joh Makini.

No comments:

Post a Comment