Monday, 4 July 2016

VYAMA VYA SIASA ZANZIBAR KUHAKIKIWA

MSA1


Bi. Esther Mwanri, Mwanansheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mara baada ya zoezi la uhakiki  katika ofisi iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. stori & picha na :ORPP
MSA2
Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bi. Monica Mwailolo (kushoto) akikagua taarifa za Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati wa zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Magomeni Jijini Dar es salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nancy Mrikalia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Augustine Mrema.
MSA3
Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akielezea jambo wakati wa zoezi la uhakiki ulioanyika katika Ofisi za Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD). Kulia ni Mwenyekiti  Taifa wa chama hicho Bw.Kamana Masoud na  Kushoto ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa” Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma”” Bibi. Piencia Kiure
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Leo imekamilisha zoezi la kuhakiki vyama vya siasa 21 kwa upande wa Tanzania Bara . Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa visiwani Zanzibar litaanza  Julai 11 mwaka huu.
Uhakiki wa Vyama utafanyika katika Ofisi za Vyama zilizopo Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba, zoezi hilo litajumuisha uhakiki wa idadi ya wanachama ambao Chama cha Siasa kinapaswa kuwa nao kwa mujibu wa masharti yalipo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa yam waka 1992.
Ikumbukwe kuwa ,zoezi hili ni moja kati ya shughuli za kawaida za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambalo hufanyika maramoja kila mwaka likilenga kufahamu utekelezaji wa masharti na matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.

No comments:

Post a Comment