July 31 2016 mwili wa marehemu Mwanahabari Joseph Senga
umeagwa Dar es salaam kuelekea Mwanza kwa ajili ya maziko, baadhi ya
viongozi wa serikali na siasa wameshiriki wakiwemo Waziri wa habari,
utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na wengine.
Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea
September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa ambaye alifariki July 28 2016 akiwa India kwa matibabu ya ugonjwa
wa moyo.
Ayo TV imefanya exclusive interview na ndugu wa marehemu Joseph Malumbete ambaye walikuwa wote hadi umauti ulipomfika ambapo anasema…
>>’Marehemu
alikuwa na tatizo la moyo, madaktari walidai mrija wa moyo ulikuwa
mkubwa hivyo walitoa mshipa mmoja kutoka kwenye mguu na kuuweka kwenye
moyo‘ –Joseph Malumbete
‘Siku ya mwisho tulikaa
kitandani akaniomba nimtengenezee dawa ili anywe lakini kabla sijaanza
akaniambia anajisikia vibaya, akawa anazidi kuishiwa nguvu, nilikuwa
peke yangu nikimhudumia‘ –Joseph Malumbete
‘Baada
ya kuona amezidiwa niliomba gari ili kumkimbiza hospitali wakati huo
hata kuongea alikuwa hawezi, baada ya kufika hospitalini wakaniambia
kuwa alishafariki muda mrefu‘ –Joseph Malumbete
No comments:
Post a Comment