Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano uliopewa jina la 2016 Mobile 360 Series Africa |
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ijulikanayo; ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28) unahofahamika kama 2016 Mobile 360 Series – Africa ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya mawasiliano, Tanzania imeungana na mataifa ya Nigeria na Ethiopia ambayo kwa utatu wao yanachukua zaidi ya theluthi moja ya soko la aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi huku kukiwa na idadi kubwa ya watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa Mawasiliano ya simu za mikononi Duniani ujulikanao kama GSMA umebaini.
Ripoti hiyo pia iliangazia mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
“Zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’ alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara, serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni 150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
No comments:
Post a Comment