Wednesday, 6 July 2016

Rihanna afuta ziara akihofia virusi vya Zika

Rihanna afuta ziara akihofia virusi vya Zika

Mwanamuziki wa kizazi kipya Rihanna amekataa kutumbuiza mashabiki wake nchini Colombia kwa kuhofia kuambukizwa virusi vya Zika.
Waandalizi wa tamasha la Lollapalooza Colombia wamejipata taabani baada ya kipusa huyo kukataa katakata kuhudhuria tamasha hilo licha ya kuwa maelfu ya mashabiki walikuwa tayari wamekwisha nunua tiketi zao.
Wanamuziki wengine waliopaswa kutumbuiza katika tamasha hilo Lana Del Rey, Disclosure, The Chainsmokers na Wiz Khalifa.
''Baada ya kujiondoa kwa nyota wa muziki wa Pop Rihanna, hatuna budi kufutilia mbali tamasha zima, hata hivyo tunawaomba radhi mashabiki wetu kwa tukio hilo na tungependa kuwahakikishia nyote kuwa gharama ya tiketi zote zilizokuwa zimenunuliwa zitalipwa.''
Msemaji wa Lollapalooza Colombia aliwaambia wahandishi wa habari za burudani.
Japo Rihanna hakuwa ametajwa rasmi kuwa mwanamuziki huyo aliyelazimisha tamasha hilo kufutiliwa mbali Waandalizi wa tamasha hilo wamewataka wafadhili wao wawawie radhi kwa sababu ambazo hazingeepukika.
Aidha tamasha hilo la Lollapalooza Colombia lilikuwa limeratibiwa kufanyika katika mji mkuu wa Bogota, Colombia.
Shirika la Afya duniani WHO lilitangaza ugonjwa wa Zika kuwa janga la umma mnamo mwezi februari mwaka huu baada ya mlipuko wa maradhi hayo nchini Brazil na haswa eneo zima la kusini mwa Marekani.
Virusi vya Zika havimdhuru mtu wala kumsababishia maradhi lakini virusi hivyo vimeonesha madhara makubwa kwa wanawake wajawazito
Tahadhari hiyo ya shirika la afya duniani liliibua hofu miongoni mwa wanariadha wanaopaswa kushiriki katika michezo ya Olimipiki mjini Rio De Janeiro kuanza mwezi ujao nchini Brazil. kitovu cha maambukizi hayo.
Virusi vya Zika havimdhuru mtu wala kumsababishia maradhi lakini virusi hivyo vimeonesha madhara makubwa kwa wanawake wajawazito ambao wengi wamejifungua watoto wenye vichwa vidogo kuliko inavyopaswa.
Aidha virusi hivyo vimebainika kusalia katika manii ya wanaume kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment