Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 06
2016 amehutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika
kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.
Katika
hotuba yake amemupongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin
Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na
ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.
Dkt.
Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza
la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za
kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi
mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.
Aidha Rais
Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha
taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema
serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba
wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.
No comments:
Post a Comment