Monday, 4 July 2016

Mji wa Medina washambuliwa

Mripuko mkubwa umetokea katika mji wa Medina nchini Saudi Arabia,shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mtu aliyejitoa muhanga alifyatua kitufe cha kujilipulia karibu na msikiti mkubwa wa Mtume, ambapo msikiti huo ni mmoja wapo ya eneo takatifu kwa Waislamu.
Kituo cha runinga mjini Saudia kilionesha picha za moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kwenye maegesho ya magari huku magari yakiteketea na mwili mmoja wa binaadamu ulionekana karibu yake.
Mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia kuhusiana na tukio hilo,tukio jingine limetokea huku mtu mwingine wa kujitoa muhanga akiwa amejiripua katika msikiti wa madhehebu ya Shia upande wa Mashariki mwa mji wa Qatif, na mripuko wa tatu umetokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Jeddah.
Askari wawili wa kulinda usalama wamejeruhiwa katika mojawapo ya matukio hayo.Mpaka wakati huu hakuna taarifa zozote kuhusiana na kundi lililo husika kupanga na kutekeleza mashambulizi hayo .Lakini kumekuwa na wasi wasi huenda wapiganaji wa Islamic State wakawa wanahusika.
Kumekuwa na shutuma kuwa utawala wa Saudia kuwa sio wa halali na ambapo wamekuwa wakiiushambulia ufalme huo mara kwa mara katika siku za nyuma.bbc

No comments:

Post a Comment