Mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliohusika katika shambulio lililotekelezwa karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu mnamo Jumanne aliwahi kuwa mbunge.
Salah Nuh Ismail, 57, alikuwa miongoni mwa watu 13 waliofariki kwenye milipuko miwili iliyotokea karibu na uwanja wa ndege, kundi la al-Shabab lilisema.
Alijulikana sana kama Badbado, jina ambalo maana yake ni ‘Usalama’ au ‘Yule Salama’.
Alijiunga na Bunge la Somalia mwaka 2000 lakini akajiuzulu na kujiunga na al-Shabab mwaka 2010.
Anakumbukwa sana kwa kuwaita wabunge wenzake “makafiri”, baada yake kujiunga na kundi hilo la Kiislam. kutoka BBC
No comments:
Post a Comment