Thursday, 28 July 2016

Kala Jeremiah aeleza uhusiano wake na Mh.Lowassa,wana mipango yoyote?


Wiki kadhaa zilizopita kwenye mitandao ya kijamii kulienea picha ya Kala Jeremiah na Roma wakiwa pamoja na waziri mkuu mstaafu Mh.Lowassa ambapo watu walidhani pengine kuna project inakuja.

Alipoulizwa kuhusiana na picha hiyo kwenye mahojiano yake na TBC,Kala alidai hakuna kitu chochote special kwenye picha hiyo na kudai kwamba yeye na Mh.Lowassa ni marafiki na huwa wanakutana mara kwa mara kushirkishana mipango yao.
Mimi na Mh.Lowassa ni marafiki tu wa kawaida,wakati mwingine tunatembeleana tunajadili vitu tu vya kawaida vya kijamii wakati mwingine sio kitu special kihivyo..tunakaa kama marafiki,kama ndugu huwa atunashirikishana mambo mbalimbali tunayotaka kufanya” alieleza Kala ambaye hivi karibuni ameachia Wimbo wake mpya unaoitwa Wana Ndoto.

1 comment: