Jumatatu ya June 13 2016 timu ya taifa
ya Hispania ambao ndio Mabingwa watetezi wa Kombe la Euro, walishuka
dimbani kutetea taji lao hilo, kwa kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kund D
dhidi ya timu ya taifa ya Czech Republic.
Katika mchezo huo ambao wengi walikuwa
wanaangalia Hispania ambaye Bingwa mtetezi wa Kombe hilo, amefanikiwa
kuanza kwa ushindi kwa kuifunga Czech Republic kwa goli 1-0, goli ambalo
lilifungwa dakika ya 87 na beki Gerrard Pique.
Licha ya Hispania kupata ushindi mdogo,
walikuwa wanamiliki mpira kwa kwa asilimia 68 na Czech asilimia 32
pekee, kadri muda wa mchezo ulivyokuwa unaenda ndio Czech walivyokuwa
wanazidi kushambuliwa kutoka na Hispania kuzidi kutawala mchezo na
kulazimisha kupata goli dakika za lala salama.
No comments:
Post a Comment