Nyota wa Kagera Sugar Juma Jabu akiwa na mkewake baada ya kufunganaye ndoa
Beki wa kushoto wa kutumainiwa wa Kagera Sugar Juma Jabu, ameuaga
ukapera baada ya kufunga ndoa na kuanza maisha maisha mapya ya ndoa
katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Juma Jabu amepambana kuisaidia Kagera Sugar kukwepa mkasi wa kushuka
daraja msimu uliomalizika mwezi May ambapo timu hiyo ilikuwa kwenye
ukanda wa kushuka daraja kwa muda mrefu.
Golikipa wa Mbeya City Juma Kaseja ambaye walicheza pamoja wakati
wakiitumikia klabu ya Simba SC alikuwepo pia kushuhudia tukio hilo
muhimu katika maisha ya Jabu. Juma
Jabu (katikati) akiwa na Juma Kaseja (kulia) ambaye walicheza pamoja
kwenye kikosi cha Simba kabla ya kuachana na klabu hiyo
Jabu ameisaidia Kagera Sugar kumaliza katika nafasi ya 12 ikiwa na pointi zake 31 baada ya michezo 30 ya VPL.
No comments:
Post a Comment