Wednesday, 11 May 2016

SIMBA SC YAIKATALIA MAJIMAJI SONGEA, SARE 0-0

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akisalimiana na wachezaji wa Simba kabla ya mchezo huo


SIMBA SC imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji, Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Majimaji, Songea jioni ya leo.
Matokeo hayo yanaiongezea kila timu pointi moja, Simba SC ikifikisha 59 baada ya kucheza mechi 28 n imebakiza michezo miwili na Majimaji 34 baada ya kucheza mechi 29 na imebakiza mechi moja.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ngole Mwangole wa Mbeya, aliyesaidiwa na Hussein Amiri na Alphaxad Mtete, timu zote zilishambuliana kwa zamu ingawa hayakuwa mashambulizi ya kusisimua.
Makipa wote, Peter Manyika wa Simba na David Burhan wa Majimaji hawakuwa na wakati mgumu katika mchezo wa leo kutokana na kutosukumiwa michomo ya hatari au sekeseke langoni mwao.
Kikosi cha Majimaji kilikuwa; David Burhan, Godfrey Taita, Mpoki Mwakimuke, Bahati Yussuf, Lulanga Mapunda, Samir Luhava, Iddy Kipagwile, Hassan Hamisi, Peter Mapunda, Marcel Boniventura na Luka Kikoti.
Simba SC; Peter Manyika, Hassan Isihaka, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Mohammed Fakhi, Novaty Lufunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mussa Mgosi, Said Issa na Peter Mwalyanzi/Justice Majabvi dk57 na Mohammed Mussa/Hussein Magila dk82.

No comments:

Post a Comment