Baada ya waziri
mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria
kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini
ikiwa matamshi hayo ni ya kweli.
Je Nigeria imeorodheshwa katika
nafasi ipi katika orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa shirikisho la
kupambana dhidi ya ufisadi duniani Transparency International ?Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa 2015 ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi, Transparency International, ili kukupa taswira ya mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani katika mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa Nigeria sio taifa fisadi zaidi duniani.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi mkubwa hata kuishinda Nigeria.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini, Eritrea, Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania Ethiopia na kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika nafasi ya 167.
Viwango vya ufisadi vinanasibishwa na Korea Kaskazini.
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya Afrika Mashariki na kati ni Rwanda.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe aliyewadunisha wakenya kwa kuwa wezi ?
Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika la TI Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.
Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / North Korea
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Democratic Republic of the Congo / Chad / Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda
No comments:
Post a Comment