Sunday, 15 May 2016

MECHI YA MAN UNITED V BOURNEMOUTH YAFUTWA, SABABU ZA KIUSALAMA!


OLDTRAFFORD-ABANDONEDMECHI ya BPL, Ligi Kuu England, kati ya Manchester United na Bournemouth iliyokuwa ichezwe Uwanjani Old Trafford imefutwa kwa sababu za kiusalama.
Mechi ni ya mwisho ya Ligi kwa Timu hizo mbili na imefutwa baada ya kugundulika kwa mzigo wa mashaka kwenye Jukwaa la Stetford End na kuwafanya Walinzi kuwatoa nje ya Uwanja Mashabiki waliokuwa Jukwaani hapo pamoja na wale wa Jukwaa la Sir Alex Ferguson huku Polisi na Mbwa spesho wa Polisi wakipita kila sehemu kuchunguza.
Baada ya muda mfupi Washabiki wakatangaziwa kuwa Mechi hiyo imefutwa na haijajulikana lini itachezwa.
Man United walikuwa wanahitaji kushinda Mechi hii na Man Cuty kufungwa hii leo ili waipiku Man City katika Nafasi ya 4 ili wacheze UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hadi Mapumziko City wakicheza Ugenini huko Liberty Stadium walikuwa Sare 1-1 na Swansea City.
LIGI KUU ENGLAND

No comments:

Post a Comment