Tayari Ligi Kuu ya Uingereza Bingwa tumeshafahamu ni klabu ya Leicester City ambayo
imeweka historia mpya, baada ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza
katika historia yake toka ianzishwe miaka 132 iliyopita, licha ya kuwa
mchezo kati ya Liverpool na Chelsea ulikuwa ni mchezo mkubwa na umemalizika kwa sare ya goli 1-1.
Huku magoli yakifungwa na Eden Hazard kwa upande wa Chelsea dakika ya 32 na Christian Benteke akaisawazishia Liverpool dakika ya 90 na kufanya vilabu hivyo kumaliza mchezo huo kwa sare ya 1-1. Stori kubwa ilikuwa katika mchezo wa Sunderland dhidi ya Everton, huo ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Sunderland kupata ushindi ili kutoshuka daraja.
Sunderland walikuwa
nyumbani na walilazimika kupambana kufa na kupona na hatimae kupata
ushindi goli 3-0, ushindi ambao ulirejesha furaha kwa mashabiki wao kama
vile wametwaa Kombe la Ligi Kuu, baada ya ushindi huo sasa vilabu vya Newcastle United, Aston Villa na Norwich City ambao leo walipata ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Watford wameshuka daraja.
No comments:
Post a Comment