Klabu ya soka ya Leicester
City wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia
kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea
siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi
kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.
Lakini wamepoteza michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu Spurs,Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.
''Kwa kigezo cha soka la ndani,Leicester City kushinda taji la ligi kuu ni mafanikio makubwa sana katika historia na haiwezi kusahaulika'' kiungo wa zamani wa Leicester Robbie Savage ameiambia BBC.''Ni jambo la ajabu.Hii ni hatua ya mageuzi katika historia ya Ligi Kuu."
Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni kama hadithi za kale.
No comments:
Post a Comment