Sunday 29 May 2016

D’banj kuifikisha mahakamani kampuni inayomiliki mtandao wa simu,kisa…!!


Kupitia account yake ya mtandao wa twitter,staa wa miondoko ya Afro-Pop ambae pia ni Host wa show ya “Lip Sync” inayorushwa na kituo cha televisheni cha  MTv,D’Banj amedai kuwa yupo mbioni kuifikisha mahakamani moja ya kampuni inayomiliki mtandao wa simu nchini Nigeria kwa madai ya kampuni hiyo kujinufaisha kibiashara kupitia kazi zake za kisanaa bila kuzingatia makubaliano na hakimiliki ya kazi hizo.
D banj post on globalcom
Hata hivyo kampuni  inayotuhumiwa na Mwanamuziki huyo inatajwa kuwa ni Globacom,kampuni ambayo D’Banj alikua balozi wake ambapo tangu mkataba wake ulipoisha kama balozi wa mtandao huo,hajasaini mkataba na kampuni nyingine.
BEST DBANJJJJHatua ya Mwanamuziki hiyo imekuja ambapo pia tarehe 4 ya mwezi May mwka huu,alitangaza kusitisha mkataba wake kama balozi wa kinywaji cha “Ciroc Vodka”huku tetesi zikidai kuwa yupo kwenye mpango wa kuzindua brand ya kinywaji chake binafsi.
SONY DSC
D’banj & Kanye West.

No comments:

Post a Comment