Meneja wa Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, alisema hali hiyo itaweza kuondoa migongano baina ya wakulima, vyama vya msingi vya ushirika na wanunuzi, wakati wa mauzo ya mazao hayo na malipo.
Alisema hayo jana wakati alipokuwa akiitambulisha taasisi hiyo ya serikali kwa viongozi wa ngazi ya ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya, makundi ya wakulima, kamati ya muda ya chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao juu ya kusimamia kimauzo mazao hayo katika msimu wa mwaka huu.
Shirima alisema uanzishwaji wa soko la bidhaa utaweza kuleta mawasiliano na sekta za fedha, miundombinu na mfumo wa stakabadhi kwa baadhi ya mazao.
Alisema kwamba maendeleo hayo yanatoa fursa za kuboresha mfumo wa masoko nchini ili kuleta mfumo wenye ushindani na ulio wazi na ambao utaweza kumfanya mkulima aweze kunufaika na juhudi zake.
Kwa mujibu wa Shirima, licha ya kuondoa migongano itaweza kuleta chachu kwa wakulima kuweza kuzalisha kwa wingi kutokana watakuwa na masoko mbalimbali ya mazao hayo.
Naye mchambuzi wa fedha wa mamlaka hiyo Witness Gowelle, alisema mamlaka hiyo isimamie kwa mara ya kwanza kwa mazao ghafi na kutafitiwa masoko.
No comments:
Post a Comment