![]() |
UEFA yaipiga marufuku Galatasaray |
Klabu ya Uturuki
Galatasaray imepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano yeyote
yalioandaliwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA kwa kipindi cha
miaka miwili kwa kukiuka kanuni za uadilifu wa kifedha
(financial fair play).Mabingwa hao wa soka ya Uturuki walisajili hasara kubwa iliyolazimu UEFA kuchukua hatua baada ya ufichuzi mwezi Januari.
Galatasaray ilifuzu kwa hatua ya makundi katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya msimu uliopita.
Vigogo hao wa soka ya Uturuki wanashikilia nafasi ya 5 hivi sasa katika jedwali la ligi kuu.
Msimu huu wanacheza katika ligi ya daraja la pili yaaani Europa ambapo waliambulia kichapo mikononi mwa Lazio.
No comments:
Post a Comment