![]() |
Kocha wa Twiga Stars Nasra Mohamed akizungumza baada ya mechi |
Timu ya taifa ya
wanawake ya Tanzania imelazwa na Zimbabwe kwenye mechi ya kufuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016.
Twiga Stars wamechapwa 2-1 na Zimbabwe katika mechi iliyochezewa uwanja wa Azam complex jijini Dar es Salaam.Magoli ya Zimbabwe yamefungwa na mchezaji Elina Jeke mabao yote mawili nalo bao la Twiga Stars likatiwa kimiani na Mwanahamisi Omar.
No comments:
Post a Comment