JUMAMOSI
huko Signal Iduna Park Mjini Dortmund Nchini Germany upo mtanange mkali
kati ya Magwiji wa Soka wa Nchi hiyo, Borussia Dortmund na Bayern
Munich, ikiwa ni Mechi ya Ligi ya Bundesliga ambayo jina lake la ubatizo ni ‘Der Klassiker’.
Bayern,
ambao ndio Mabingwa Watetezi na wanaoongoza Ligi wakiwa Pointi 5 mbele
ya Dortmund, wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kwenye kipigo cha
kustukiza cha 2-1 kutoka kwa FSV Mainz ambacho walikipata wakiwa
Nyumbani kwao.
Dortmund wao walishinda Ugenini 2-0 Siku hiyo hiyo Jumatano kwa kuifunga SV Darmstadt 98.
Katika Mechi ya kwanza ya Bundesliga Msimu huu iliyochezwa huko Allianz Arena, Munich, Bayern Munich iliinyuka Dortmund 5-1.
Lakini
safari hii, Dortmund haitakuwa ubwete baada ya kuonyesha maendeleo
mazuri sana huku Mchezaji wao kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang,
akiwa amepiga Bao 22 kwenye Bundesliga akiwa Bao 1 tu nyuma ya Straika
hatari wa Bayern Robert Lewandowski.
BUNDESLIGA
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Machi 5
1730 VfB Stuttgart v TSG Hoffenheim
1730 SV Werder Bremen v Hannover 96
1730 VfL Wolfsburg v Borussia Monchengladbach
1730 Eintracht Frankfurt v FC Ingolstadt 04
1730 FC Koln v Schalke 04
1730 FC Augsburg v Bayer 04 Leverkusen
2030 BV Borussia Dortmund v Bayern Munich
Jumapili Machi 6
1730 FSV Mainz 05 v Darmstadt
1930 Hamburger SV v Hertha Berlin
No comments:
Post a Comment