Monday, 22 February 2016

Marekani na Urusi kusimamisha vita Syria

Marekani na Urusi zimetangaza kusimamisha vita nchini Syria kuanzia usiku wa Ijumaa.
Makubaliano hayo yametangazwa baada ya mawasiliano kwa njia ya siku kati ya Rais Barack Obama na mwenzake Vladimir Putin.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Staffa de Mistura amesema changamoto kubwa ni kuhakikisha makubalino ya kuacha vita yanatekelezwa katika uwanja wa vita.
Makundi mawili ya wapiganaji wenye itikadi kali ya kiislamu Islamic State na Al- Nusra Front hayapo kwenye makubaliano hayo.
Muungano wa upinzani nchini Syria umesema kujihusisha kwao kutategemea jinsi gani serikali ya Syria na washirika wake watakavyoacha kuuzingira, kuwafungulia wafungwa na kuacha kupiga mabomu.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia anasema ukurasa huu mpya kutaipa ugumu Urusi kuwapiga mabomu wapinzani ambao sio waislamu wanaungwa mkono na mataifa ya Magharibi na baadhi ya nchi maarufu za Kiarabu.

No comments:

Post a Comment