Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amewafuta kazi takriban watu ishirini na sita ambao ni wakuu wa idara mbali mbali za serikali ikiwemo vyombo vya habari.Maafisa hao wametakiwa kukabidhi madaraka kwa maafisa wa ngazi za juu katika idara zao mpaka kutakapofanywa uteuzi mwengine.
Huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yanatarajiwa kuathiri zaidi ya mamia ya idara za serikali.Rais Buhari amepata shinikizo kubwa la kufanya mabadiliko hayo ambayo yangewaachisha kazi maafisa wengi ambao walikuwa karibu na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan. Nafasi zao zinatakiwa zichukuliwe na wafuasi kutoka chama cha APC, hasa wale waliokuwa na mchango mkubwa katika uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Buhari.

No comments:
Post a Comment