Monday, 22 February 2016

Man United walicheza usiku wa February 22 FA Cup dhidi ya Shrewsbury, video ya magoli hii




Baada ya Jumapili ya February 21 kuchezwa michezo mitatu ya Kombe la FA na kushuhudia Chelsea ikiiondoa Man City kwa jumla ya goli 5-1, usiku wa February 22 klabu ya Man United ilishuka dimbani kuchuana na klabu ya Shrewsbury Town katika mchezo wao wa Kombe la FA.
5184
Man United ambao walikuwa ugenini waliibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli ya Man United yalianza kufungwa dakika ya 37 na Chris Smalling, kabla ya dakika nane mbele kiungo wa kimataifa wa Hispania Juan Mata kupachika goli la pili kwa kupiga mpira wa faulo kifundi na kutinga wavuni na  dakika ya  71  Jesse Lingard akahitimisha kwa kufunga goli la tatu. 


No comments:

Post a Comment