Sunday, 21 February 2016

Kama ulikuwa hufahamu, hii ndio list ya viwanja 10 vyenye thamani zaidi Afrika, uwanja wa Taifa upo pia


Huenda ukawa upo Tanzania lakini hili ukawa hulifahamu tumezoea kusikia kuwa Tanzania ni nchi ambayo inatambulishwa vivutio vya utalii hususani mlima Kilimanjaro. February 22 katika pitapita zangu www.sportstardom.com nimekutana na list ya viwanja 10 vilivyojengwa kwa gharama kubwa barani Afrika. Naomba nikusogezee list yenyewe mtu wangu na uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ukitajwa katika list hii.
10- Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam huu ulijengwa kwa dola milioni 53 na nusu ya hela za ujenzi huo zilitolewa msaada na serikali ya China. ulifunguliwa mwaka 2007 na unauwezo wa kuchukua mashabiki 60000.
Benjamin_Mkapa_National_Stadium
9- Stade Olympique de Radès huu ni uwanja uliopo Tunisia mji wa Rades, uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni sawa na uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, ila gharama yake inatajwa kufikia dola milioni 110, ulijengwa mwaka 2001.
Stade_Olympique_De_Rades
8- Mbombela Stadium ni moja kati ya viwanja vilivyotumika katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini, kina thamani ya dola milioni 140, kina uwezo wa kuchukua mashabiki 40,929.
Mbombela_Stadium
7- Peter Mokaba Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, ulijengwa kwa dola milioni 150 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 41,733, kwa sasa unatumiwa na klabu ya Black Leopards FC kama uwanja wa nyumbani.
Peter_Mokaba_Stadium
6- Estádio 11 de Novembro upo Angola lakini ulitumika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010, umejengwa kwa dola milioni 227 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.
Estadio_11_De_Novembro
5- Nelson Mandela Bay Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270 upo katika mji wa Port Elizabeth na unauwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake limetoka na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela.
Nelson_Mandela_Bay_Stadium
4- Abuja Stadium hiki ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa kwa gharama zaidi barani Afrika, dola milioni 360 ndio zilitumika kujenga uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,491 upo  mji mkuu wa Nigeria Abuja.
Abuja_Stadium
3- FNB Stadium ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 440, ulichezewa fainali za Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini. FNB Stadium jina lake lilizoeleka na wengi ni Soccer City. Huu ndio uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi zaidi barani Afrika, unauwezo wa kubeba watu 94,736.
FNB-Stadium
2- Moses Mabhida Stadium ulijengwa kwa dola milioni 450 , uwanja huu upo Durban Afrika Kusini na ulitumika kwa baadhi ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia 2010, ulikuwa na uwezo wa kuingia mashabiki 62,760 lakini wakati wa fainali za Kombe la Dunia ulipunguzwa na kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 54000.
Moses_Mabhida_Stadium
1- Cape Town Stadium huu ndio uwanja wenye thamani kuliko vyote barani Afrika, kwani zimetumika dola milioni 600, unauwezo wa kuingia mashabiki 64,100.
Cape_Town_Stadium

No comments:

Post a Comment