
FC Midtjylland, Kitimu cha Denmark kilichoanzishwa Mwaka 1999 chenye Uwanja MCH Arena unaochukua Watu 11,800, Leo kimeichapa Manchester United Bao 2-1 katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA EUROPA LIGI

Man United walitangulia kufunga lakini udhaifu wa Kiungo na Difensi yao uliruhusu FC Midtjylland kupiga Bao 2 na kuwa na nafasi kadhaa za kuongeza Bao nyingine kadhaa.

man United, wakiwakosa Wachezaji wao kadhaa kutokana na maumivu, walipata pigo kabla Mechi hii kuanza baada ya Kipa wao David de Gea kuumia Enka wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero.

MAGOLI:
FC Midtjylland 2
-Pione Sisto, Dakika ya 44
-Ebere Paul Onuachu 77
Man United 1
-Memphis Depay, Dakika ya 37

EUROPA LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Februari 16
Fenerbahce 2 Lokomotiv Moscow 0

Alhamisi Februari 18
Sevilla 3 Molde 0
Villarreal 1 Napoli 0
Borussia Dortmund 2 Porto 0
Anderlecht 1 Olympiacos 0
Fiorentina 1 Tottenham 1
St Etienne 3 Basle 2
Midtjylland 2 Manchester United 1
Valencia 6 Rapid Vienna 0
Augsburg 0 Liverpool 0
Sparta Prague 1 Krasnodar 0
Galatasaray 1 Lazio 1
Sion 1 Braga 2
Shakhtar Donetsk 0 Schalke 0
Marseille 0 Athletic Bilbao 1
Sporting Lisbon 0 Bayer Leverkusen 1
**Mechi za Marudiano ni Februari 25.
KALENDA
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Kwanza: 18 Februari
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Pili: 25 Februari
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
No comments:
Post a Comment