
Vikosi vya Usalama
nchini Misri vimewapiga risasi washukiwa wawili wa Islamic State baada
ya kuvamia hoteli moja kwenye mwambao wa bahari nyekundu ya Hurghada.
Watali 3 kutoka Ulaya walijeruhiwa katika shambulio hilo ,baada
ya wanamgambo hao kuingia kwenye hoteli na kuwakabili wageni huku
wakipeperusha bendera nyeusi ya IS .
Eneo la tukio hilo lilifungwa kwa uchunguzi.
Ni
shambulio la pili katika eneo hilo linalopendwa na watalii hasa nyakati
za mapumziko ambapo shughuli za utalii zimedorora tangu kudunguliwa kwa
ndege ya Urusi mwezi Novemba mwaka jana na kile ambacho IS ilitaja kuwa
ni bomu
No comments:
Post a Comment