Mahakama hiyo pia imemwamuru mshtakiwa huyo kuilipa serikali kiasi cha Sh bilioni 1.2, ikiwa ni fidia ya kuua tembo hao. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Januari mosi, mwaka huu kijijini Nsenkwa wilayani Mlele.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa, alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Wankyo Simon kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Tengwa alisema ametoa hukumu hiyo, ili iwe fundisho kwa mshitakiwa mwenyewe na wengine wanaojihusisha na ujangili wa meno ya temb
No comments:
Post a Comment