Kama unadhani unamjua sana Young Killer basi haya ni mambo 3 ambayo hauyajui kuhusu yeye.
1) Young Killer na mpenzi wake Miss Hiphop wamezaliwa siku moja ambayo ni April 13 lakini wamezaliwa miaka tofauti. Ukipita kwenye page ya Young Killer utakutana na picha za mpenzi wake huyo maarufu kwa jina la Miss Hiphop.
2)Simu yake ya kwanza kuanza kutumia ambayo ni Nokia ya tochi anayo hadi leo. Anachokifanya ni kubadilisha housing tu na kuendelea kuitumia kama kawaida. Licha ya kuwa na simu mpya nyingine lakini bado anaendelea kutumia simu hiyo.
3)Kama asingekua msanii wa Hiphop basi leo hii angekua anacheza soka. Young Killer anasema yeye alikua na ndoto kubwa kwenye soka zaidi ya muziki. Young Killer anasema kwamba aliwai kupitia kwenye academy ya soka ya kocha maarufu marehemu Sylvester Mash huko Mwanza.
No comments:
Post a Comment