UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mechi za Mwisho za MakundiRATIBA
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumatano Desemba 9
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Barcelona Roma v BATE Borislov
KUNDI F
Dinamo Zagreb v Bayern Munich
Olympiakos v Arsenal
KUNDI G
Chelsea v FC Porto
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv
KUNDI H
KAA Gent v Zenit Saint Petersburg
Valencia v Lyon
ARSENE WENGER amesisitiza Arsenal wanaingia Jumatano Uwanjani Karaiskaki huko Piraeus, Ugiriki kuwavaa Olympiakos katika Mechi ya mwisho ya Kundi F la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL ambayo lazima washinde ili wafuzu Raundi ya Mtoano ya Timu 16, wakiwa hawaogopi kitu.
Lakini si ushindi tu bali wanapaswa kuipiku Rekodi ya Olympiakos waliyoiweka Emirates ambako waliichapa Arsenal 3-2 katika Mechi ya kwanza.
Hivyo, ikiwa Arsenal watashinda kwa Bao 1-0 au 2-1 watatupwa nje.
Ikiwa Arsenal hawatafuzu basi watatupwa nje na kulazimika kucheza UEFA EUROPA LIGI kwa vile watakuwa Nafasi ya 3.
KUNDI: F:
Olympiacos (Pointi 9) v Arsenal (6)
Dinamo Zagreb (3) v Bayern München (12, Imeshafuzu)
-Bayern ndio Mabingwa wa kundi.
-Olympiacos
waliifunga Arsenal 3-2 huko Emirates na hivyo Arsenal wanatakiwa wapate
ushindi bora zaidi ya huo dhidi ya Olympiakos watakapokutana huko
Athens.
-Dinamo wako nje.
Arsenal wamefuzu kucheza Raundi ya Mtoano ya UCL kwa Miaka 15 mfululizo hadi sasa lakini hali ngumu ya sasa kwenye Kundi lao halikumfadhaisha Meneja wao Arsene Wenger ambae amejipa moyo.
Wenger amesema: “Tutafanya kila jitihada tufuzu. Ukitaka kuruka kihunzi hufikirii nini kitatokea ukikosea!”
No comments:
Post a Comment