Monday, 7 December 2015

LIVERPOOL NAO WAPATA KIPIGO KITAKATIFU ANGALIA HAPA NIMEKUWEKEA KILA KITU YA VIDEO YAKE


December 6 ni siku ambayo mechi za Ligi Kuu Uingereza za weekend hii zilichezwa za mwisho, mchezo ambao ulikuwa una funga mechi za weekend ya December 6, ilikuwa ni mechi ya kati ya Newcastle United dhidi ya majogoo wa jiji Liverpool katika dimba la St James Park.
1897
Liverpool wakiwa ugenini wamekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa wenyeji wao Newcastle United, Liverpool ambayo inafundishwa na kocha wa kijerumani Jurgen Klopp ilianza kuruhusu goli la kwanza dakika ya 69 kipindi cha pili, baada ya beki wao Martin Skrtel kujifunga goli na kuifanya Newcastle kupata goli la kuongoza.
2735
Goli la kujifunga la Martin Skrtel lilifanya mchezo uzidi kuwa mgumu kwa upande wa Liverpool, kwani licha ya kujitahidi kutaka kusawazisha walijikuta dakika ya 90 Georginio Wijnaldum akiwafunga goli la pili, goli ambalo liliiwezesha Newcastle United kuvuna point zote tatu katika dimba lake la nyumbani St James Park.

No comments:

Post a Comment