Wanamuziki Justin
Bieber na Taylor Swift ndio waliotamba zaidi kwa mazungumzo katika
mtandao wa kijamii wa Twitter mwaka 2015, wakuu wa Twitter wamesema.
Kwa miezi sita ya kwanza, Taylor Swift ndiye aliyetawala kabla ya Justin Bieber “kuchukua usukani”.Lakini mazungumzo katika mtandao wa Twitter haujakuwa kuhusu wasanii pekee na muziki.
"Mazungumzo ya kisiasa na watu wakieleza hisia zao pia vimeongezeka,” mkuu wa Twitter Ulaya Bruce Daisley aliambia kipindi cha Newsbeat.
"Ndiye msanii wa tatu kwa kuwa na wafuasi wengi Twitter. Nusu ya pili ya mwaka, Justin Bieber alitawala,” anasema Daisley.
"Bieber ndiye wa pili kwa kuwa na wafuasi wengi. Alikuwa na wafuasi 50 milioni na amewatumia vyema na kwa werevu.”

No comments:
Post a Comment