Wednesday, 2 December 2015

CAPITAL ONE CUP: LEO ‘WATAKATIFU’ NA LIVERPOOL, DROO YA NUSU FAINALI BAADA YA MECHI HIYO!

Image result for SIGN OF CAPITAL ONE
Capital One Cup Robo Fainali

**Mechi kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumatano Desemba 2

Southampton v Liverpool

Wakati Leo ipo Mechi ya mwisho ya Robo Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, wakati Timu za Ligi Kuu England pekee zitakapocheza. Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’ na Liverpool, Droo ya Mechi za Nusu Fainali itafanyika mara tu baada ya Mechi hii.
Jana Everton, Manchester City na Stoke City zilitinga Nusu Fainali baada ya kushinda Mechi zao za Robo Fainali.
Hivyo, Timu hizo 3 na Mshindi kati ya Southampton na Liverpool watumbukizwa kwenye Droo hii ya Nusu Fainali.
Mechi za Nusu Fainali huchezwa kwa mikondo miwili, ya Nyumbani na Ugenini, na zitachezwa kwenye Wiki ya kuanzia Tarehe 4 Januari 2016 na Marudiano kufanyika Wiki ya kuanzia 25 Januari 2016.
Capital One Cup
Robo Fainali
Matokeo:
Jumanne Desemba 1
Middlesbrough 0 Everton 2
Stoke City 2 Sheffield Wednesday 0
Manchester City 4 Hull City 1

No comments:

Post a Comment