Usiku wa November 25 ilipigwa michezo ya mechi za klabu Bingwa barani Ulaya, lakini usiku wa November 26 ilikuwa ni zamu ya muendelezo wa mechi za michuano ya UEFA Europa League, klabu ya Liverpool ambayo inashiriki michuano hiyo ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Bordeaux katika dimba la Anfield
Liverpool ambao wapo chini ya kocha wao mpya mjerumani Jurgen Klopp waliingia katika dimba lao la nyumbani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa goli 4-1 kutoka katika mchezo wao wa Ligi Kuu Uingereza iliyocheza dhidi ya Man City katika uwanja wa Etihad, Liverpool ilianza kwa kuruhusu kufungwa goli na Bordeaux dakika ya 33 kupitia kwa Henri Saivet.
Livepool ambao kwa muda
mrefu walikuwa wanaongoza kumiliki mpira, walifanikiwa kusawazisha goli
hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 38 kupitia kwa James Milner, Liverpool waliongeza mashambulizi na dakika ya 45 Christian Benteke akapachika goli la pili na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-1. Licha ya Bordeaux walionesha jitihada za kutaka kusawazisha goli kipindi cha pili, mchezo ulimazika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-1.



No comments:
Post a Comment