UEFA CHAMPIONZ LIGI
MATOKEO:
Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF 0 Paris St Germaine 5
Shakhtar Donetsk 3 Real Madrid 4
KUNDI B
CSKA Moscow 0 VfL Wolfsburg 2
Man United 0 PSV Eindhoven 0
KUNDI C
FC Astana 2 Benfica 2
Atletico Madrid 2 Galatasaray 0
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach 4 Sevilla 2
Juventus 1 Man City 0
KATIKA Mechi za 5 za Maundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zilizochezwa Usiku huu huko Ulaya, Juventus, Paris Saint Germaine, Benfica na Atletico Madrid zimefanikiwa kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zikiwa na Mechi 1 mkononi.
Timu hizi zinaungana na Real Madrid, Man City na Zenit Sainta Petersburg, zilizofuzu mapema pamoja na Barcelona na Bayern Munich zilizotinga Raundi ya Mtoano Jumanne Usiku.
Real Madrid, wakicheza Ugenini huko Ukraine na wakiwa tayari wameshafuzu, waliongoza 4-0 hadi Dakika ya 76 kwa Bao za Cristiano Ronaldo, Bao 2, Luka Modric na Carvajal lakini ndani ya Dakika 11 Shakhtar Donetsk wakapiga Bao 3 na gemu kwisha 4-3.
Ushindi huu wa 4-3 kwa Real umewafanya wamalize Kundi A wakiwa Washindi wa Kundi na kufuatiwa na PSG walioifunga Malmo 5-0 huko Sweden huku Zlatan Ibrahimovic akipiga Bao dhidi ya Timu yake ya Nyumbani kwao aliyochipukia nayo.
Huko Turin, Italy, Mario Mandzukic aliifungia Bao Juventus walipoifunga Manchester City 1-0 na kufuzu pamoja na Man City ambao walikuwa tayari wamefuzu kabla ya Mechi hii.
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA MTOANO:
**Bado 7
Real Madrid
Paris St-Germain
Atletico Madrid
Benfica
Juventus
Manchester City
Barcelona
Bayern Munich
Zenit St Petersburg
No comments:
Post a Comment