Saturday, 24 October 2015

NIMEKUWEKEA MATOKEO YA REAL MADRID NA CELTA VIGO






Ligi Kuu Hispania imeendelea tena leo October 24 kwa michezo kadhaa kupigwa nchini Hispania, klabu ya Real Madrid ya Hispania ilikuwa mgeni wa Celta Vigo katika uwanja wa Estadio Municipal de BalaĆ­dos uwanaja ambao  Celta Vigo wanautumia kama uwanaja wao wa nyumbani.









1718426-36366913-640-360
Real Madrid ambao walikuwa ugenini kucheza na Celta Vigo, wamefanikiwa kuondoka na point tatu muhimu katika mchezo huo. Real Madrid ikiwa na mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo alifanikiwa kupachika goli dakika ya 8 na kuifanya Madrid iongoze. Furaha ya Real Madrid iliendelea baada ya  Danilo kupachika goli la pili dakika ya 23.
3000
Celta Vigo ambao walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani walifanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 85 kupitia kwa Nolito ila Marcelo dakika ya 90 akafunga goli la tatu, hivyo hadi dakika 90 zinamalizika Real Madrid ilifanikiwa kuifunga Celta Vigo jumla ya goli 3-1

No comments:

Post a Comment