
Kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’
Simba kikiwa katika maandalizi ya kuwavaa ‘wagosi wa kaya’ Coastal Union
siku ya Jumatano, hali ya majeruhi Hamisi Kiiza imezidi kuimarika na
yupo tayari kuongoza mashambulizi ya kikosi cha Dylan Kerr.
Mtandao huu umemtafuta daktari wa
Simba SC Yasin Gembe ambaye amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa
kusema baada ya kupata matibabu, raia huyo wa Uganda yuko tayari kucheza
mchezo dhidi ya Coastal Union.
“Kiiza sasa hivi yuko sawa, tangu
alipopata ‘injury’ alikuwa anahitaji wiki tatu au zaidi lakini ndani ya
wiki tatu ameonesha ‘recovery’ ya kutosha, ameshaanza mazoezi tangu
wiki iliyopita kwahiyo mwalimu kama atamuhitaji anaweza kumtumia kwenye
mechi ijayo”, amesema Gembe.
“Mbali na Kiiza wachezaji wengine
wako vizuri isipokuwa kwa Faki ambaye alikuwa na maumivu ya goti kwa
muda mrefu na ni mchezaji pekee ambaye hayupo kwenye kambi lakini
wengine wote wapo kambini”.
Urejeo wa Hamisi Kiiza kwenye
kikosi cha Simba ni habari njema kwa mashabiki wa Simba ambao walimkosa
kwenye michezo mitatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment