
Everton 1 Norwich City 1 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Everton 4 Norwich 3]
Hull City 0 Leicester City 0 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Hull 5 Leicester 4]
Sheffield Wednesday 3 Arsenal 0
Stoke City 1 Chelsea 1 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Stoke 5 Chelsea 4]
SHEFFIELD WEDNESDAY 3 ARSENAL 0
Sheffield Wednesday, Timu inayocheza Daraja la chini la Championship, imeitwanga Arsenal Bao 3-0 na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi liitwalo Capital One Cup.
Bao za Sheffield zilifungwa na Ross Wallace, Dakika ya 27, Eduardo Lucas Joao, 40, na Sam Hutchinson, 51.
VIKOSI:
Sheffield Wednesday: Wildsmith, Hunt, Lees, Loovens, Pudil, Wallace, Lee, Hutchinson, Bannan, Helan, Lucas Joao.
Akiba: Palmer, Semedo, Nuhiu, McGugan, Bus, Sasso, Price.
Arsenal:
Cech, Debuchy, Chambers, Mertesacker, Gibbs, Flamini, Kamara, Oxlade-Chamberlain, Iwobi, Campbell, Giroud.
Akiba: Gabriel, Walcott, Monreal, Macey, Bielik, Bennacer, Sheaf.
REFA: Graham Scott
STOKE CITY 1 CHELSEA 1
Stoke City wamewatupa nje Mabingwa Watetezi wa Capital One Cup Chelsea kwa kuwatoa kwa Mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo huu wa Raundi ya 4 ya Kombe hili.
Stoke City walitangulia kufunga katika Dakika ya 52 kwa Bao la Jonathan Walters na Chelsea kusawazishia katika Dakika ya 91 baada ya Mpira wa Kona na Loic Remy kufunga.
Dakika za Nyongeza 30 hazikuzaa Goli licha ya Stoke kucheza Mtu 10 baada ya Beki wao Phil Bardsley kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika za Majeruhi ya Dakika 90 za mwanzo.
Stoke walisonga baada ya kufunga Penati zao zote 5 za mwanzo na Chelsea kukosa Penati yao ya 5 wakati Shuti la Eden Hazard lilipookolewa na Kipa Jack Butland.
Ushindi huu umewaingiza Robo Fainali.
VIKOSI:
Stoke: Butland; Bardsley, Shawcross, Wollscheid, Muniesa; Whelan, Adam; Diouf, Afellay, Arnautovic; Walters.
Akiba: Given, Ireland, Odemwingie, Wilson, Sidwell, Shaqiri, Crouch.
Chelsea: Begovic; Zouma, Cahill, Terry, Baba Rahman; Ramires, Mikel; Willian, Oscar, Hazard; Costa.
Akiba: Amelia, Loftus-Cheek, Azpilicueta, Remy, Kenedy, Traore, Djilobo
No comments:
Post a Comment