Monday, 9 December 2013

TANZANIA YA ADHIMISHA MIAKA 52 YA UHURU KWA KUOMBOLEZA MSIBA WA MANDELA


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi MkuuDkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Kikosi cha Jeshi la  Wanamaji.
 Jana Watanzania wameadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zamani Tanganyika huku dunia ikiendelea kuomboleza kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyefariki dunia jijini Johannesburg wiki iliyopita. Akizungumza katika maadhimisho hayo Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa taifa la Tanzania litaendelea kumkumbuka shujaa huyo wa Afrika kutokana na mchango wake katika kupigania uhuru wa wananchi wa Afrika Kusini

Rais Kikwete amesema kuwa Mzee Mandela alikuwa mtu wa kipekee kutokana na ujasiri wa kutetea haki za wanyonge licha ya kupata mateso kutoka kwa makaburu.

Hayati Mandela atakumbukwa kwa moyo wa kusamehe na kupinga ubaguzi wa Rangi akiwa katika harakati za ukombozi na hatimaye Afrika Kusini ikawa huru.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam ambapo Rais Kikwete alikagua gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama.

Tanzania Bara ilipata uhuru wake mwaka tarehe 9 Desemba 1961 kutoka kwa wakoloni wa Uingereza na Baba wa Taifa hilo Hayati Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa harakati zake za kuhakikisha Taifa hilo linakuwa huru.

Kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika kwa mwaka huu inafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu.

No comments:

Post a Comment