Friday, 6 December 2013

KITUO CHA KUTOA USAIDIZI WA KISHERIA KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA CHA ZINDULIWA


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Kusaidia walioathirika na Ukatili wa kijinsia kituo ambacho kinajulikana kwa jina la One Stop Center kilichojengwa katika hospitali ya Amana kwa ufadhili wa shirika la fhi. Tukio hilo limefanyika siku ya jana Alhamisi mchana. jijini Dar es Salaam



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akisikiliza maelekezo kutoka kwa watoa huduma wa kituo cha  One Stop Centre kitakachokuwa kinatoa msaada wa kisheria na ushauri kwa waathirika wa Ukatili wa Kijinsia

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa dawati la jinsia kutoka jeshi lapolisi, wizara ya afya na shirika la fhi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kutolea huduma kwa waathirika wa Ukatili wa Kijinsia jana jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. na kifanye kazi kama kilivokusudiwa...zama za ukatili zilikwisha pita

    ReplyDelete