Friday, 1 November 2013

HALIMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI IMETOA WITO KWA WAKAZI WA MANISPAA HIYO KUJENGA UTAMADUNI WA KUSHIRIKI KATIKA VIKAO NA SHUGHULI ZA KISERIKALI


Akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari maelezo afisa Uhusiano wa manispaa ya Kinondoni Bw Sebastian Mhowera ametoa wito huo kwa kusema kua wananchi wanatakiwa kushiriki katika vikao na shughuli za kiserikali ili kuongeza kasi ya mafanikio yaliyopo na pia kuimarisha umoja na mshikamano katika kutatua kero zilizopo pamoja na kutafuta mfumo unaofaa katika uendeshaji wa halmashauri

Pia bwana Mhowera amesema kua miongoni mwa faida zinazo tokana na ushiriki wa wananchi katika vikao na shughuli za ki serikali ni pamoja na
Kuimarika kwa mawasiliano kati ya wananchi na serikali,
 Kuelewa mafanikio na changamoto zilizopo, uwepo wa uhuru wa kutoa maoni na mapendekezo katika uendeshaji wa serikali
 na wananchi kuelewa mfumo wa uendeshaji wa serikali kutoka katika ngazi za mitaa mpaka manispaa

Aidha bwana Mhoera amebainisha  kua kwa kuzingatia umuhimu wa ushiriki wa wananchi  katika vikao na shughuli za ki serikali manispaa ya kinondoni ime andaa mazingira mazuri ya vikao hivyo na shughuli za kiserikali kutokana na ukweli kua ushirikiano kati ya serikali na wananchi ni njia mojawapo ya kuleta mabadiliko ya haraka katika maendeleo


No comments:

Post a Comment