| Theresa May ndiye waziri mkuu wa Uingereza |
Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza.
Akizungumza
baada ya kupokea ufungua wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza
10 Downing Street bi May amehakikishia washirika wake na mataifa ya
muungano wa ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa,Uingereza inapania kujiunga na mataifa shirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano wa mataifa huru duniani.
Amesema kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio wachache na kusahau wananchi wa kawaida.
Aliwakumbusha wakosoaji wake maana ya jina rasmi ya chama chake ambacho ni chama cha Conservative and Unionist.
Waziri huyo mkuu ameapa kuangamiza udhalimu wa aina yeyote ima ni kwa misingi ya ubaguzi wa rangi jinsia ama kiwango cha mapato.
Bi Theresa May ni waziri mkuu wa 13 kuwahi kuiongoza Uingereza katika enzi ya Malkia Elizabeth wa pili.
Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.
No comments:
Post a Comment