Waziri Nape Nnauye akimkabidhi cheti bondia Francis Cheka baada ya kushinda ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super middle wa WBF.
Waziri Nape Nnauye akiuvaa mkanda
wa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super middle wa WBF mara baada ya
kukabidhiwa na bondia Francis Cheka.
……………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia Francis “SMG” Cheka kwa
kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super-Middle wa chama cha WBF baada
ya kumtwanga kwa pointi bondia Mserbia, Geard Ajetovic.
Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.
Akitoa pongezi hizo jana, Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa Rais
amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeipa heshima nchi katika
medani ya michezo ndani na nje ya mipaka yake.
Waziri Nnauye alisema kuwa
serikali imeweka utaratibu wa kuwapongeza wanamichezo wanaofanya vyema
kimataifa ili kuleta hamasa kwa wengine na wale wanoafanya vizuri
kuongeza bidii.
“Cheka umefanya mambo makubwa
sana, umeiletea sifa Tanzania na Rais amefuraishwa sana, naomba kuongeza
bidii na wengine kufuata nyayo zako, nimefurahi kusikia kuwa mdogo
wako, Cosmas naye ameshinda ubingwa wa Afrika, nampongeza sana,” alisema
Nnauye.
Katika hafla hiyo, Serikali
ilimpa cheti cha pongezi Francis Cheka na kumtaka kuzidi kuitangaza nchi
kupitia mchezo huo ambao ni wa kwanza katika historia ya Tanzania
kuleta heshima. “Serikali inaahidi kusaidia mchezo na mabondia ili
kufikia maendeleo ya juu kabisa,” alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Cheka aliipongeza serikali na kutambua mchango wake katika kuleta sifa
ya nchi hii na kuahidi kuleta mikanda mingi ya ubingwa wa dunia.
“Nimefurahi kutambuliwa na serikali, nimepata hamasa kubwa sana, naahidi kufanya mambo makubwa katika mchezo huu,” alisema.
Mkurugenzi wa Advanced Security,
Juma Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka alisema kuwa wamefarijika sana
kupata pongezi za serikali na kuahidi kuandaa mapambano mengi ya Cheka
kwa mabondia wan je ya chi katika mapambano ya ubingwa wa Dunia.
No comments:
Post a Comment