Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo za Grammy alifariki akitibiwa katika hospitali moja mjini Los Angeles, Alhamisi usiku.
Alikuwa amefutilia mbali tamasha kadha, ikiwemo ya mkesha wa Mwaka Mpya.
Cole alipata umaarufu kama mwimbaji wa R&B kwa nyimbo kama vile This Will Be na Inseparable.
Mtetezi wa haki za kiraia wa Marekani Kasisi Jesse Jackson alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutuma salamu za rambirambi.
Mwanamuziki huyo aliwahi kutatizwa na matumizi ya dawa za kulevya na ugonjwa wa hepatitis awali, na alibadilishwa figo mwaka 2009.
Albamu hiyo ilishinda tuzo sita za Grammy, zikiwemo tuzo za albamu bora ya mwaka, na wimbo bora wa mwaka. CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment