Monday, 23 November 2015

SELE ASHINDA SURA MBAYA ZIMBABWE

hini Zimbabwe kumefanyika mashindano ya kipekee ya kumpigia kura mwanaume mwenye sura mbaya zaidi katika taifa hilo.

Kama mashindano mengine ya urembo shindano hili pia lilivutia washiriki wengi na Jopo la majaji lilikua na mengi ya kutahini richa ya sura walitizama hulka na kujitanua kwa washindani

cha kushangaza katika mashindano hayoKihoja kilizuka pale waamuzi walipomtaja Mison Sere, kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe.

Hata hivyo mashabiki wa bingwa mtetezi,William Masvinu walilalamikia uamuzi huo wakidai kuwa bwana huyo alikuwa na sura nzuri tu licha ya mwanya mkubwa na tabasamu kama ya kibogoyo.

Licha ya majibizano makali Sere mwenye umri wa miaka 42 alituzwa mshindi na kutuzwa dola mia tano ($500).Yeye na mke wake walishangilia tuzo hilo jukwaani na kuwatonesha kidonda wafuasi wa mpinzani wake waliowazomea na hata kuzua vurugu wakidai kapendelewa.

'Walihoji umauzi wa majaji wakisema kuwa hakuwa na sura mbaya ila alikuwa ka'ngoa meno yake ya mbele.''Inakuwaje wanampuuza bingwa wa zamani William Masvinuambaye maumbile yake yanatisha mno'' wali lalamika mashabiki.

Bingwa mara tatu wa tuzo la mtu mwnye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe William Masvinu alikwenda nyumbani katika nafasi ya pili.

'Huyu bwana hatishi kamwe,hebu tizama pua langu kubwa uso wangu mweusi na unavyotisha,sikio langu ni kama la popo ni kubwa itakuwaje kuwa amenishinda ?'

'La sikubaliani na uamuzi huu wa leo, nimeudhika sana.'' Masvinu alisikika akinungunika.

No comments:

Post a Comment